Thursday 15 May 2014

HUU NDO UJUMBE KWA WANAOTUMA UJUMBE WA NGONO - KENYA


Kumtumia mtu ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini Kenya kunaweza kukuweka mashakani.
Maafisa wakuu wanasema kuwa yeyote atakeyepatikana na hatiaatafungwa jela kifungo cha miezi mitatu kwenda chini...

Afisaa mkuu kutoka tume ya kitaifa ya mawasiliano, Christopher Wambua ameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono pamoja na picha zenye watu walio uchi watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au dola miatano na themanini na nane kama faini au kufungwa jela..
Onyo hilo litawaandamana hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya mkononi au kwenye internet.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali, kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za, smartphone ilipanda hadi asilimia sitini.
bbcswahili.com

0 comments :

Post a Comment