Monday 28 October 2013

HATIMAYE MTU MREFU KULIKO WOTE DUNIANI APATA MKE..TAZAMA PICHA HAPA..



kwa urefu inawezekana akawa kamzidi mkewe kwa futi mbili na nusu au zaidi..Lakini “ Sultan Kosen” mtu mrefu kuliko wote duniani ana furaha kwa kumpata mke wake wa ndoa..kijana huyu anataraji kumuoa “Merve Dibo” baada ya kuhangaika mda mrefu akitafuta mpenzi wa kuishi nae maishani..Tazama picha zingine hapa chini..

Kosen ambaye ni mkulima kutoka Uturuki ameiambia Reporter wa AA kua anafarijika atakua na familia yake sasa na kuishi maisha yao binafsi..pia aliongezea kua hakuweza kumpata mwanamke wa urefu wake lakini anaamini huyu ndiye mwanamke sahihi kwake..
Kosen anashikilia rekodi ya Guiness ya mtu mrefu kuliko wote duniani mwaka 2009 kwa kua na urefu wa futi 8  na inchi 3 baada ya kumshinda Bao Xishun kutoka china(futi 7 na inch 9).
Suti pamoja na viatu vya harusi vitatengenezwa maalum kwa ajili ya sherehe hiyo..

0 comments :

Post a Comment