Saturday 30 November 2013

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KIMEPATA VIONGOZI WAPYA WATAKAONGOZA KWA MWAKA 2013-2014..


                                 Dennis Muhazi

Serikali ya wanafunzi ya chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) inafuraha kubwa ya kuwapata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika jana chuoni hapo.. Katika uchaguzi huo kuna Post tatu ambazo zilikua Zikishindaniwa, ambazo ni: Rais , Makamu wa Rais na Waziri Mkuu (General secretary)....endelea hapa chini..
Katika sehemu iliyokua na upinzani mkubwa ni nafasi ya Urais iliyokua na washindani watatu, Timoth Msigwa, Salim Othman na Denis Muhazi ambapo Bwana Denis Muhazi amefanikiwa kunyakua kiti cha urais baada ya kuwapiku wapinzani wake kwa Kura zaidi ya 200...


Cosmas Muhanuzi

Katika post nyingine iliyokua ikipambaniwa ni uwaziri mkuu(general secretary)  iliyokua na Wapinzani wawili , Frank Lymo na Cosmas Muhanuzi ambapo Bwana Cosmas Muhanuzi amefanikiwa kushinda kiti hicho kwa kumuacha mpinzani wake kwa kura zaidi ya 400..

Katika post ya tatu ya Kumtafuta  Makamu wa Rais ambayo post hiyo walikua wakichuana Madada watatu, Sophia Watosha, Agness Malebeto na Ruth Nkonoki..nafasi hiyo ilichukuliwa na mwanadada Sophia watosha kwa kuwapiku wenzake kwa kura Zaidi ya 200...
 

 uongozi Mzima wa PLANET CHOICE unayofuraha kuwapongeza washindi wote na inawatakia mema katika shughuli zao za ujenzi wa taifa..




0 comments :

Post a Comment