Monday 21 July 2014

YANGA YAMSAJILI RAIA MWINGINE WA BRAZIL..

Mshamabuliaji Geilson Santos Santana “Jaja” raia wa
Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili

(2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans
Jaja akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu
Katibu mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema
usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa
wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo
mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa
Brazil.
“Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha
mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo
ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada
kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu
kiende safi” alisema Beno.
Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na
kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka
anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa
akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari
alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki iliyopita chini
ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake
Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha
Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali.

0 comments :

Post a Comment