Sunday 10 November 2013

KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI.. WATOTO HAWA WANAHITAJI MSAADA WAKO..

KIBOWA ni kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu(yatima).. jina KIBOWA ni ufupisho wa maneno “Kituo Bora cha Watoto”..Kituo hichi kilichopo Lemara jijini Arusha lina Watoto Takribani 49 na  kimekua kikiendeshwa na
WAnamama wawili ambao hupitia mihangaiko mingi katika kufanikisha mahitaji ya watoto hawa kwani ukizingatia hawana chanzo chochote cha kuwaingizia mapato(wanaendesha kwa kutegemea misaada kutoka kwa watu mbali mbali)..




Katika mengi yaliyosemwa na Walezi wa Kituo hicho ni mahihitaji makubwa ya misaada  na walijaribu kutuelezea changamoto nyingi ambazo wanakutana nazo.. Ni dhahiri kua wengi Tunajua Mazingira halisi ya watoto kama hawa na inahitaji moyo wa kujitolea ili kufanikisha malengo ya Watoto hawa ambao wana ndoto za kufika mbali kimaisha..
Pamoja na Mengi yaliyofanywa na wanafunzi hao .pia walijumuika katika Mlo wa Pamoja na watoto hao…


 


                                                 Shughuli zingine nazo ziliendelea pia....

 wanafunzi wa Uhasibu wakibadilishana mawazo na Mama Mlezi(mama Miraji)


                           Hizo baadhi ya picha za pamoja zilizochukuliwa Kituoni Hapo...


Tafadhali Ndugu ,Jamaa, Marafiki uliyejisikia Kuguswa na Maisha ya watoto hawa ..Tunaomba kwa Moyo wa Dhati, mchango/msaada wako wa aina yoyote ile na kwa Kadri utakavyoweza ili tuweze kufanikisha malengo mazuri waliyonayo watoto hawa…Tunaomba kama Umeguswa na unajisikia kutoa chochote Tafadhali Wasiliana na kiongozi atakeyekujulisha jinsi ya Kufikisha Mchango wako Kwa namba ZIfuatazo..(+255659085236 Gama Mwende)..
Kumbuka: Mchango wako ni wa Msaada sana kwa Watoto hawa na tunakaribisha mawazo/michango mbali mbali katika kutimiza ndoto za watoto hawa…
Give a man fish and you feed him for a Day, Teach a Man How to Fish and you feed him for a Life Time..

0 comments :

Post a Comment