Monday 21 October 2013

IRENE PAUL KUOLEWA BILA MAHARI...



Stori: Imelda Mtema...

MKALI wa sinema za Kibongo, Irene Paul amesema wakati wake wa kuolewa ukifika, hatatolewa mahari kama ilivyozoeleka badala yake atachukuliwa bila ya mume
kugharamia.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Irene alisema linapokuja suala la kuolewa huwa haoni maana ya mahari kwani mahari inayotolewa haiwezi kufika hata theluthi ya malezi ambayo wazazi walimlea.

“Kama tumeafikiana kuoana na mchumba wangu sitahitaji mahari kabisa maana kwa upande mwingine naona kama ni kutugeuza kama watumwa sisi wanawake,” alisema Irene Paul.

0 comments :

Post a Comment