Tuesday 29 October 2013

HUYU NDO JAMAA MWENYE MUSTACHI MREFU DUNIANI..AMETUMIA MIAKA 32 KUFUGA MUSTACHI HUO



Ni mzee wa miaka 58 “Ram Singh Chauhan” kutoka jaipur  huko Rjasthan nchini india… ni mzee mwenye mustachi mrefu duniani na amekua akiufuga mustachi huo kwa miaka 32 sasa..Mustachi wake una urefu wa futi 14 na hutumia mda wa masaa mawili kuzisafisha…

Chauhan amepata umaarufu kupitia mustachi wake na ilifanya akaigiza kwenye muvi ya james bond “Octopussy”..pia aliongeza kua, kufuga mustachi ni kama kumlea mtoto inabidi kumtunza sana..imenichukua mda mrefu kuzifikisha futi 14 na sio kazi rahisi hata kidogo-alisema Chauhan.
Alianza kufuga mustachi akiwa na umri wa ujana na hajawahi kuzinyoa toka miaka ya 1970..alisema mustachi ni ishara ya heshima na mustachi una maana sana kwake

0 comments :

Post a Comment