Saturday 14 September 2013

BABY MADAHA ASAINI MKATABA WA SHILINGI MILL 50 KENYA



 Staa wa muziki wa Bongo Fleva na filamu,Baby Madaha amelamba bingo ya uhakika na kampuni
ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.

Meneja wa msanii huyo Joe Kariuki amesema kuwa pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa million hamsini (50) pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT na nyumba kali mitaa kijitonyama jijini Dar es salaam.…
 
Baby madaha ambaye anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya wimbo wake wa kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko huko jijini Naironi.
SOURCE: Bongomovies.com

0 comments :

Post a Comment