Friday 30 August 2013

HII INAMAANISHA NO BEEF KATI YA MADAM RITA NA NEY WA MITEGO

 


Ni mengi umeyasikia wakati huu ikiwa ni siku kadhaa tu baada ya kutoa single ambayo amechana
baadhi ya watu maarufu kwenye burudani na siasa Tanzania ambao Ney wa Mitego mwenyewe anasema lengo ni kufanya hivyo ili wajirekebishe.
Moja kati ya stori zilizotokea ni pale aliposema Madame Rita Paulsen amekwenda kumshitaki Mahakamani kisa katajwa kwenye wimbo ambao Ney aliuliza pesa za washindi wa BSS zinakwenda wapi, pia washindi hawafanikiwi kimaisha baada ya kutoka kwenye shindano hilo la kusaka vipaji vya uimbaji.
Sasa basi…… Ney wa Mitego na Madam Rita si wakakutana jana August 29 2013 kwenye uzinduzi wa video ya Diamond…………. unadhani walichuniana au kununiana? big Nooooo!!!!! walisimama, wakakumbatiana baada ya kuongea na hatimae kupiga picha ya pamoja wakiwa wanatabasamu…..
hii ilitokana na habari ambazo zilivyoandikwa ilionekana ni beef kati yao wawili manake Madame baadae alikanusha na kusema hakwenda kushtaki kokote na hawezi kufanya hivyo kwa sababu kwanza kilichosemwa na Ney sio kitu cha kupeleka na pia hajawahi kukutana na Ney na wala hamjui hata kwa sura.




 

 

0 comments :

Post a Comment