Friday 23 May 2014

HII NDO KAULI YA WAYNE ROONEY ENDAPO VAN PERSIE ATAKUA NAHODHA WAKE ..

372816_heroa 
Tangu Nemanja Vidic alipotangaza rasmi kwamba msimu ujao hatokuwepo Old Trafford msimu ujao, kulianza tetesi juu ya mchezaji gani atapewa nafasi ya kurithi mikoba ya unahodha ya Vidic.

Wayne Rooney mmoja wa wachezaji wakubwa ndani ya klabu ya Manchester United alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha mpya wa United wakati timu hiyo ikiwa chini ya David Moyes, lakini baada ya kutimuliwa kwa kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Louis Van Gaal, mshambuliaji wa kiholanzi na nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi Robin van Persie amekuwa akipewa nafasi ya kumrithi Vidic, huku Van Gaal akisema kwamba yeye na RVP wana filosofia moja hivyo wanakuwa na urahisi wa kufanya kazi pamoja na kama kocha na nahodha wake.
Hali hiyo imepelekea Wayne Rooney ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya unahodha msimu ujao kuzungumza: “Navutiwa na suala la kuwa nahodha,” alisema Rooney kwenye mkutano wa waandishi wa habari.   

“Nimeshewahi kuwa anahodha wa muda United kwa mara kadhaa na kupata jukumu hilo moja kwa moja litakuwa jambo zuri sana.”

Akizungumzia suala la Van Persie kupewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha ajaye wa United, Rooney alisema:

“Ikiwa kocha wetu atamchagua mtu mwingine, then kiukweli kabisa sitokuwa na tatizo na hilo. Nitaheshimu maamuzi yake. 

“Robin ni nahodha wa nchi yake, ameshawahi kuwa nahodha wa Arsenal na ikiwa atapata nafasi hiyo United, basi kwa hakika naamini atafanya kazi nzuri.”

0 comments :

Post a Comment