Saturday 8 March 2014

HUU NDIO UJIO MWINGINE WA ROMA MKATOLIKI...K.K.K...



Bila Shaka Watu wengi Mnahamu sana Ya kusikia Ujio wangu Mpya na Pia utakuwa na Maswali Mengi sana Kichwani kwako kuwa Hivi sasa Nimezungumzia nini, Kama Ilivyo kawaida ya Muziki wangu ni Kupigania na Kutetea Haki za Wanyonge, 


K.K.K ni wimbo ambao pia Unatetea haki za Walio wanyonge Wanao hangaika na Kuelemewa na Mizigo ya Shida. Pia kama ilivyokuwa Katika Wimbo wangu wa 2030 uliweza kumsikia Mtoto Mdogo Story na ukaanza kumfahamu na Kumjua baada ya Ngoma ile kutoka, Sasa na Hii K.K.K utaweza Kumsikia Kijana mwingine Mpya ...

Nia na Lengo ni Kutoa Msaada kwa wasanii Chipukizi ambao wanafanya Vizuri.

Kazi nzima ya wimbo Huu imefanyika Pale Tongwe Rec, Kama ilivyo kawaida yangu, J3 utaweza Kuisikia katika Media Nyingi za Hapa Bongo pamoja na Mikoani Maana Ndio siku Maalum ya Kuachia Ngoma hii iliyo subiriwa kwa Muda Mrefu, Naomba Muipokee na Kusapoti Harakati.

0 comments :

Post a Comment