Tuesday, 13 August 2013

ROBERT MUGABE AMWAMBIA MPINZANI WAKE MORGAN TSVANGIRAI AKAJINYONGE

Rais wa zimbabwe Robert Mugabe amemwambia mpinzani wake Morgan Tsvangirai akajinyonge.. Mugabe alisema kua hawezi kurudi nyuma baada ya kushinda matokeo ya uchaguzi nchini humo na pia Rais huyo wa zimbabwe aliongezea kua wale wote wanaodai uchaguzi haukua wa haki waende wakajinyonge.
 http://nehandaradio.com/wp-content/uploads/2012/07/Mugabe-Tsvangirai-590-e1342524722888.jpg
mapema katika hotuba yake mara  baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo july 31, Mr Mugabe
mwenye umri wa miaka 89 alisema "yeye na chama chake cha Zanu PF wameshinda uchaguzi kwa kura za wananchi na sio kwa vita na alishukuru nchi jirani za Afrika kwa kulitambua hilo na kukubaliana na uchaguzi huo".
Mugabe alisema " tumepigana kiume kwenye uchaguzi huu na tumeshinda, na watu wengine wameumia vibaya " aliiambia umati wa watu ulokusanyika eneo hilo kuichukua siku hiyo kama siku ya mashujaa na kusherekea kila mwaka kwa ajili ya wale wote waliopigania uhuru wa zimbabwe(zamani Rhodesia) kutoka kwenye mikono ya wakoloni..

0 comments :

Post a Comment