Duniani kuna maajabu mengi,kati ya maajabu hayo ni
huu mgahawa uitwao Rock uliopo visiwani Zanzibar uliojengwa juu ya mwamba
mkubwa katika bahari ya Hindi..
Tazama picha zaidi hapa chini...
Mgahawa huo ulifunguliwa rasmi mwaka jana na kuna
viti 45 ambapo wateja huchukuliwa na boti maalum kutoka pwani hadi kupata
huduma katika mgahawa huo ili wasikanyage maji wakati wakiingia kwenye mgahawa
huo.
Chakula
kinachopatikana muda wote katika mgahawa huo ni samaki pekee kutoka baharini na
vinywaji.
Wafanyakazi
wa The Rock
The Rock umetajwa kuwa ni mgahawa wa ajabu katika
Afrika Mashariki na watu wengi wakiwemo watalii hupenda kwenda kutokana na
habari zake kuenenea kwa kasi na wengi hupendelea kupata hewa safi ya baharini
na kuona jinsi kilivyokuwa ndani.
Rock, ambayo ilifunguliwa mwaka jana, inaweza kufikiwa
kwa miguu, lakini pia kuna usafiri wa mashua wa kuwasafirisha wateja kutoka
pwani hadi kwenye mgahawa huo.
teentz.com
0 comments :
Post a Comment