Tuesday, 22 July 2014

REAL MADRID YAKAMILISHA USAJILI WA JAMES RODRIGUEZ KUTOKA MONACO

Real Madrid wamekamilisha usajili wa mshindi wa

kiatu cha dhahabu katika michuano ya World cup ndani ya Brazil 2014. James Rodriguez mshambuliaji kutoka Colombia ana umri wa miaka 23 na amesaini mkataba wa miaka sita na Real Madrid akitokea club ya Monaco.
Ripoti zinasema gharama ya uamisho ni pauni milioni 63 na kumfanya mchezaji wa nne wa uhamisho wa gharama akiwa nyuma ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez. Kama umesahau ni kwamba Rodriguez alifunga magoli sita katika mechi tano za world cup hadi kuifikisha timu yake ilipofika katika robo fainali.

0 comments :

Post a Comment