Brazil imemtangaza mchezaji wa zamani Dunga kuwa kocha wa timu ya
taifa, kwa mara ya pili. Dunga alikuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994
waliposhinda Kombe la Dunia, na alikuwa kocha kuanzia mwaka 2006 hadi
2011.
"Nimefurahi sana kurudi," amesema Dunga, 50, ambaye alikuwa akitajwa
sana kuchukua nafasi hiyo. Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe
Scolari, aliyejiuzulu baada ya Brazil kufika nusu fainali ya Kombe la
Dunia 2014, lakini alipata kipigo kizito katika historia ya taifa hilo kwa
kufungwa 7-1 na Ujerumani. Dunga aliifikisha Brazil katika robo fainali
Afrika Kusini mwaka 2010.
0 comments :
Post a Comment