Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na
kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo. Good news Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika mashariki na wimbo bora wa kushirikiana (Number one) ambayo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru
na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow
down’ Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben
Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wakike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril
wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka ni Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana Dj Oskido wa South Africa, Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnum
0 comments :
Post a Comment