Friday, 25 July 2014

GAZA : ISRAEL NA HAMAS WASITISHA VITA..

Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wamekubaliana kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu kuanzia leo asubuhi.

Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.
Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu
yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .
Bwana Kerry amesema atendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja
wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba
hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.


Chanzo: bbcswahili.com

0 comments :

Post a Comment