Ni longtime mwigizaji Mtanzania Jaqueline Wolper amekua kimya na
hajasikika akiyatoa ya moyoni kuhusu yote yaliyompata kwenye miezi
iliyopita na kumfanya amiliki sana headlines za magazeti, blogs, website
pia facebook na twitter huku wengi wakiwa na hamu ya kusikia
akiyaongelea.
Kwenye Exclusive interview na mtangazaji Sporah wa The Sporah show,
Jaq amekanusha kwamba yeye ni msagaji japo mara kadhaa ameonekana akivaa
kiume na kusisitiza ‘sasa hivi nimepunguza sana kuvaa nguo za kiume,
wengi walikua wanahisi lakini sijawahi kufanya vitendo vya usagaji na
wala sijawahi kushawishiwa na mtu anaejihusisha na vitendo hivyo,
boyfriend wangu hana tatizo na mavazi ya kiume ninayovaa… hatujawahi
kupangiana mavazi’
Kwenye jibu jingine alilotoa J anasema ‘sijaolewa na wala sijawahi
kuolewa, nilishawahi kubadili dini kweli… ni vitu vinatokea na
usimuhukumu mtu bila kumuuliza’
Sporah: Ni kweli kwamba
ulikutana na mtu ana uwezo wa kifedha na kulikua kuna vitu unataka
akununulie akasema hawezi kukufanyia mpaka ubadilishe dini ili upate
hizo mali?
J Wolper: ‘Sio hivyo, dini
nilikuja kubadilisha wakati nimeshapata mali, nilibadilisha mwishoni
kabisa baada ya huyu mwanaume kuja kwetu akitaka kunioa, alinipa mali na
vitu vya thamani kabla ya sisi kukutana, unajua unaweza ukawa unachat
na mtu mkapendana lakini hamjawahi kukutana… ni mzuri wa kukushawishi,
unajua sio rahisi mtu akiwa mbali aweze kukushawishi mkapendana wakati
yeye yuko mbali na wewe uko mbali, namsifia kwa uzuri wake… sio wa umbo
wala sura bali ana roho nzuri na alinitreat vizuri mpaka nikaona huyu ni
sahihi nikabadilisha dini’
Sporah: Ulifikiria kwamba dini yako sio nzuri au?
J Wolper: ‘Kwa utamaduni wetu sisi Afrika, Tanzania ninavyojua hata kwa mama yangu imetokea, Mwanamke lazima ufate dini ya Mwanaume wako’
Sporah: Lakini alikua bado hajakuoa?
J Wolper: Nilikua tayari nimeshajiona kama mke wake, ni mtu ambae alinipenda sana…
Sporah: Ulijichora na tatoo ya jina lake?
J Wolper: Kwa nini nichore jina la
mtu kwenye mwili wangu, kwanza yeye ni Muislamu hapendi tatoo…
nilibadili dini kwa mapenzi yangu mwenyewe kutokana na mtu niliekua nae
na hawajui alivyonishawishi mpaka mimi nikabadili, sio kwa
kulazimishwa….
‘Ninachojua mimi heshima ni kufata dini ya Mwanaume ukishachumbiwa,
haikua kama girlfriend na boyfriend… alikua ananifanya kama mke wake
japo hatukua tumekutana’ – J Wolper
Sporah: Ulijisikiaje pale vitu havikwenda vizuri?
J Wolper: ‘Mi naona ni sawa tu
kwa sababu Mungu pia anapanga ila sikuumia sana, ningeumia kama mimi
ndio ningekua nimetaka kuolewa ila yeye ndio alitaka ndoa, mimi bado
mdogo… watu wa mitandao kwao ni big deal ila kwangu sio kitu’
‘Haukuwa
uamuzi mgumu, napenda sana kufata moyo wangu… siwezi kufata moyo wa
mtu, wengi waliniambia sijui ukibadili dini tena sijui mashabiki wako
sijui nini nini… NOOOO! sio kuhusu mashabiki, mimi ni mimi kama mimi
sikupenda kilichotokea na bado niko chini ya wazazi wangu, vp ikitokea
nimekufa nitazikwaje sijaolewa??! mi siwezi kumchezea Mungu ndio maana
ukiangalia instagram yangu mimi kila Jumapili lazima niende kanisani’ –
Wolper
J Wolper: ‘Nilikaa miezi miwili
bila kwenda Msikitini wala Kanisani, nilikonda kwa sababu siwezi kukaa
bila kusali na wazazi wangu nakua nawakosea, kuna neno mama yangu mdogo
aliniambia baada ya kukaa na mama na kuongea nikasema ngoja nirudi
kanisani, siwezi kufaidisha watu na kuacha wazazi wangu wakasononeka…
nilibadili dini kwa heshima ya mchumba wangu lakini sasa hivi nimerudi
kwa heshima ya wazazi wangu’
J Wolper: ‘Bado Dallas ni rafiki
yangu mkubwa sana kwangu na ni mtu poa, haongei mapenzi maskini… ni
rafiki yangu ni kaka yangu, hatuwezi tena kuwa wapenzi… nampenda bado’
Unataka stori kama hizi zisikupite?...
Itazame Video Hapa chini....
1 comments :
haya mama
Post a Comment