Sunday, 6 April 2014

MASTAA WAJITONGOZESHA KWA DIAMOND PLATNUMZ... TAZAMA HAPA


KUMBE! Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’ amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo.

Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na dada yake wa hiyari, Halima Kimwana. Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima na Diamond katika pozi.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.
Diamond Platnumz akimmwagia manoti Halima Kimwana siku alipomfanyia pati.
Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.
Kama hiyo haitoshi, Halima Kimwana alianika kuwa, hajishughulishi na suala la uhusiano wa Diamond na atamheshimu kila msichana atakayetambulishwa KAMA WIFI HUKU AKITOLEA MFANO JINSI ANAVYOUHESHIMU UHUSIANO WA DIAMOND NA WEMA SEPETU KWA SASA.

0 comments :

Post a Comment