Mkali wa Hip Hop kutoka ilala Lafamilia "Chidi Benz" leo hii katika kipindi cha XXL kinachoendeshwa na clouds Fm ametangaza kuacha kutumia madawa ya kulevya, vilevi na ganja.. Chidi benz ameyasema hayo wakati alikua akitambulisha ngoma yake mpya ambayo alisema haina jina na kutaka watanzania kumsaidia kulipatia jina wimbo huo na pia Chidy alisema ni mda mrefu sasa toka aanze kutumia madawa ya kulevya, vilevi na ganja ambavyo vilikua vinamjengea sana hasira.
uamuzi huo umekuja baada ya kuona vilevi hivyo vimeanza kumzidi uwezo na alisaidiwa na mshkaji wake wa
karibu kutoka Kenya "msanii Nonini".
Chidi benz alikua kenya kwa mda mrefu sana akiwa na mwenyeji wake Nonini ambapo walikua wakifanya show nchini humo... Nonini alimwambia Chidi kua kuna njia za kuachana na madawa hayo(hakutaja ni njia gani) bila kwenda Rehab ila ni gharama na risky sana..Chidi alikubali kufanya na mpaka sasa amedai yuko vizuri na hatorudi tena kwenye madawa.
planet choice tunampongeza chidy kwa uamuzi alioufanya na tunamtakia afya njema
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment