Ndege ya Malaysia iliyokuwa imebeba abiria 295
ndani yake imeanguka Mashariki mwa Ukraine
ikitokea Amsterdam kwenda Kuala Lumpur,
kufuatia tuhuma kuwa ilitunguliwa.
Miili kadhaa ya watu imesambaa katika eneo
ilipoanguka ndege hiyo karibu na kijiji cha
Grabovo, kinachodaiwa kushikiliwa na waasi.
Ndege hiyo ya MH17 ilikuwa inakaribia kuingia
katika ardhi ya Urusi wakati ilipopoteza
mawasiliano.
Pande zote mbili serikali ya Ukraine na waasi
wamekanusha kuitungua ndege hiyo katika mji ulio
karibu na mpaka wa Urusi.
0 comments :
Post a Comment