Fifa imetangaza orodha ya majina 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia - 2014 Golden Ball.
Wachezaji watatu wametoka Argentina, Angel Di Maria, Javier Mascherano
na Lionel Messi. Mahasimu wao wa siku ya Jumapili Ujerumani, imetoa
wachezaji wanne, Mats Hummels, Toni Kroos, Phillip Lahm na Thomas
Muller.
Wengine ni James Rodriguez kutoka Colombia, Neymar wa Brazil na Arjen Robben wa Uholanzi.
Fifa
pia imetangaza majina ya watakaowania tuzo ya golikipa bora wa michuano
hiyo. Keylor Navas wa Costa Rica, Manuel Neuer wa Ujerumani na Sergio
Romero wa Argentina watawania tuzo hiyo.
Wakati huohuo Memphis Depay
wa Uholanzi, Paul Pogba na Raphael Varane wa Ufaransa wamechaguliwa
kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika Kombe la Dunia.
Washindi watatangazwa baada ya mchezo wa fainali siku ya Jumapili.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment