Mwanadada muigizaji Elizabeth Michael ametoa ushauri huu kwa wasanii pamoja na mashabiki wao baada ya kusikia wimbo mpya wa Ali kiba- mwana Dar.... Lulu aliandika hivi kwenye akaunti yake ya instagram...
Haya sasa.....maelezo hatimaye yamepatikana....mnivumilie ni marefu
Kidogo...!
1. Pongezi kwa @officialalikiba nimesikia Mwana wa Dar es Salaam tu lkn kiukweli Mimi binafsi umenikonga moyo...!
2.ieleweke kwambi Mimi ni shabiki wa mziki mzuri hata ukiwa umeibwa na underground na wengi wenu mmekuwa mashaidi maana huwa na post video nikiimba miziki ya watu tofauti hata wasio mastar wakubwa...kwahyo mm sio shabiki wa mtu ni shabiki wa kazi ya mtu
3.Nimegundua wasanii wengi wa Tanzania tuna U mimi....hivi ulaya
wangekuwa hvyo...Hollywood c kungekuwa na mtu mmoja tu au wawili
basi....nadhani umefika muda wa wasanii Kama wasanii kila mmoja
kujiamini ktk kazi Zake na kufikiria kufanya makubwa sio kufikiria kushindana na flani.....tena tukishirikiana tutaweza kufika mbali zaidi ya hapa...tutaendelea kila cku kuona maajabu wenzetu Nigeria wanafika mbali....wanajielewa na wanashirikiana...!Kama binadamu kukoseana kupo ila ukijua kosa kuomba msamaha na kuendelea na maisha ndo busara zaidi
4.Hapa sasa....nieleweke jmn...Mashabiki wetu Tunawapenda sawa....lakini kwa namna moja au nyingine Mashabiki
mnchangia bifu za wasanii....JAMANI Ukiwa shabiki wa Lulu haimaanishi
umchukie Wolper(mfano)Kama ww ni shabiki wa mtu sio umchukie
msanii mwingine na hii kwakweli ninaiona Tanzania tu(thou sio Mashabiki WOTE) 5.Mwisho...WOTE tunategemeana wasanii tupendane tukiona wenzetu flani wana shida tusaidie kuondoa tofauti na
Mashabiki pia nyie ndo msaidie kupatanisha watu sio kuchochea
ugomvi....Mungu alivyotuumba wengi alikuwa na maana yake sasa we
ukitaka uwe Mkali pekeyako ungeumbwa mwenyewe ukawekwa kwenye
dunia ya pekeyako tukusome kwenye history dunia flani Kuna mtu mkali yuko pekeyake..!duh nimechoka kuandika lkn cjamaliza.....bt I real wish wakali mngeungana mfanye mambo makubwa....naamini inawezekana...!
0 comments :
Post a Comment