Hii ni kampeni ya Rose Ndauka
ambayo kaipa jina la Ng’arisha Tanzania inayohamasisha kuweka jiji la Dar es
salaam katika hali ya usafi na kupendeza ambapo kampeni hii inahusisha kufagia
baadhi ya mitaa katika manispaa ILALA ili kuzoa taka na kuzitupa maeneo
husika.
Kampeni ilianza majira ya saa moja asubuhi na
kumalizika saa 3 asubuhi baada ya hapo ukafanyika uzinduzi wa jiko la kuchomea
taka mtaa wa Lumumba katika Manispaa ya Ilala ikiwa ni kama ishara ya
kuhamasisha raia wote Kuamka na Kubadilika na kuonyesha mapenzi kwa kuweka miji
katika hali safi kwa kusafisha maeneo wanayoishi.
Hizi ni baadhi ya picha za mastar mbalimbali wa Tanzania walivyojumuika
na Rose Ndauka katika kampeni hii.
0 comments :
Post a Comment