Ulishawahi kujiuliza kwanini video ya
Shakira na Rihanna haikuwa na model yoyote wa kiume? Inawezekana hili likawa
moja ya jibu: Gerard Pique hataki mchumba na mama wa mtoto wake Shakira afanye
video akiwa na mwanaume mwingine.
Kwa mujibu mahojiano aliyoyafanya na
jarida la Billboard Magazine,
Shakira amesema haruhusiwi kufanya video na wanaume wengine, hiyo ni amri ya
mchumba wake Pique ambaye ni mwanasoka wa FC Barcelona.
“Pique hataki nifanye video na
wanaume, ndio maana ikabidi video yetu iwe ya wanawake tu.”
Shakira aliendelea, “Hili suala
halina mjadala tena, mie nimekubaliana nalo na nimependa, anaonyesha kwamba
anapenda kulinda mali yake na ananithamini, kiasi kwamba hataki mwanaume
mwingine aushike au kutazama mwili wangu kama alivyofanya Rihanna,” alisema
Shakira huku akicheka.
0 comments :
Post a Comment