Friday, 8 November 2013

STEVE NYERERE: TUSIMLAUMU RAY..WEMA ALIKUA HAJITOI KWENYE MISIBA YA WENZAKE..

Msanii wa filamu, Steve Nyerere amesema Wema Sepetu alikuwa hajitoi kwenye matatazo ya wasanii wenzake wa filamu na ndio maana wasanii wengi wa filamu wakashindwa kuhudhuria katika mazishi ya baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu mwishoni mwa mwezi uliopita...Endelea hapa chini..

Akizungumza  leo Steve,amesema anawataka watu waache kumtupia lawama Vicent Kigosi aka ‘Ray’ wakati mwanadada huyo alikuwa hahudhurii katika matatizo ya wenzake.

“Mnamlaumu bure Ray jambo ambalo hajafanya kwakuwa Ray ni jalala basi kila kitu mnamtupia,jamani mwacheni apumzike,” amesema Steve.

“Sisi katika Bongo Movie Unity tuna uongozi, tuna mwenyekiti,tuna mwenyekiti wa mipango ambaye ndio mimi, na tuna makamu wa mwenyekiti ambaye ndio mimi na tuna makamu mwenyekiti ambaye ni Irene Uwoya. Lakini sisi taratibu zetu kwenye misiba kama unaona kwenye misiba yetu tunajitoa,lakini linavyotufika tunaangalia ni mwanachama gani naye anakua anajitoa katika misiba ya wenzake
Bongomovies.com

0 comments :

Post a Comment