Saturday, 26 October 2013

NEY WA MITEGO APIGWA MARUFUKU KUVAA MLEGEZO..

Ney wa Mitego 1

Ney wa Mitego ambae ni staa wa single za ‘muziki gani’ na ‘salamu zao’ amethibitisha kupewa barua na baraza la sanaa Tanzania ikiwa ni onyo la kutoendelea kuvaa suruali mlegezo kwenye majukwaa mbalimbali anayoonekana.

 Ney amesema alipigiwa simu sana na namba moja lakini alikua amelala, alipoamka akakuta missedcalls nyingi so ikabidi apige ndio akaambiwa BASATA kuna barua yake ambapo baada ya kushindwa kwenda alipelekewa Manzese.
Ney anasema ‘sielewe kama BASATA ndio wameamua kudili na milegezo, sijaelewa wao wanaangalia nini zaidi, nimejaribu kuuliza wakasema nikiendelea watanifungia kazi zangu, ni kweli navaa mlegezo lakini kuna vitu vingi sana vya kufanyia kazi wao kama BASATA manake tunaibiwa kazi zetu kila siku mbona hawashughulikii hizo?’ mi tangu niko shule mlegezo ni tatizo langu kubwa ila nitajitahidi kupunguza japo nashangaa nimeandikiwa barua mimi mwenyewe wakati kuna wasanii wanavaa mlegezo hata kuliko mimi’
millardayo.com

0 comments :

Post a Comment