Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa baba
mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema .A. Sepetu , “Balozi Isaac Abrahamu
Sepetu” amefariki dunia.. Marehemu
Amefariki jijini Dar-es-salaam na Mipango ya
mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini
Dar. Habari zinaeleza kuwa Mzee Isaac Sepetu alikuwa mgonjwa kwa muda wa miezi kadha hivi karibuni na amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi na kisukari.
PLANET CHOICE inaitakia pole familia nzima ya Sepetu
na Uvumilivu katika wakati mgumu kama huu..Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali
pema peponi…
0 comments :
Post a Comment