Baada ya fans wengi kuanza “kumponda” mwanadada Irene Uwoya kuwa gari aina ya Range Rover aliyoinunua “amehongwa na washika dau”, mwanadada huyo ameibuka na kusema kuwa mali anazomiliki amezinunua kwa pesa zake anazopata kwenye
uigizaji pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
“Kwa nini watu hawataki
kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi tukinunua magari tumehongwa?
Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya.
Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya
filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila
senti unayoipata, unaweza kupata mafanikio makubwa.
“Tunaigiza sehemu nyingine ambazo
hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama
ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko
kazini,” alisema
Irene amesema kuwa ameamua kuweka
wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki
amenunuliwa na wanaume ‘wanaomweka mjini’.
Bongomovies.com
0 comments :
Post a Comment