Thursday, 26 September 2013

MAHAKAMA YAKATAA RUFAA YA TAYLOR... YAWEZEKANA AKASOTA JELA KWA MIAKA 50..

Mahakama maalum ya umoja wa mataifa mjini Hague imekataa ombi la rufaa lililowasilishwa na
aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.
Jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa hukumu ya miaka 50 waliompa bwana Taylor kwa kuwasaidia waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ni ya haki.
Bwana Taylor ni rais wa kwanza wa zamani kuwahi kupatikana na hatia katika mahakama ya kimataifa tangu kesi ya Nazi.
Mawakali wake walitaka aachiliwe ,wakidai kuwa kwamba makosa ya kisheria yalifanyika wakati wa kesi yake.
Lakini upande wa mashtaka ulitaka kifungo hicho kuongezwa hadi miaka 80 jela.
SOUCE:bbcswahili.com

0 comments :

Post a Comment