Thursday, 8 August 2013

NEYMAR ARUDISHA KIASI CHOTE KILICHOTUMIKA KUMNUNUA




Mchezaji wa barcelona aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka club ya SANTOS "Neymar Da Silva Jr" amerudisha kiasi chote cha pesa iliyotumika kumng"oa kutoka club yake ya zamani ya santos kabla ya msimu wa ligi kuu barani humo kuanza...
Neymar ambaye alinunuliw kwa euro millioni 57 kutoka santos na club yake mpya ya barcelona imeshuhudia kiasi hicho chote kimerudi kutokana na mauzo ya jezi ya mchezaji huyo. Barcelona imeshuhudia mauzo ya 570,000 ya jezi yenye jina la mchezaji huyo yakilipa euro millioni 57. barca ilikua ikiuza jezi hizo kwa euro 100 kwa kila jezi..

Baadhi ya mashabiki wa barcelona wakiwa wameshikilia jezi ya Neymar.
Mpaka sasa neymar ameshacheza mechi mbili akiwa na timu yake ya barcelona na ameonekana kua na msaada mkubwa kwenye timu hiyo

0 comments :

Post a Comment