Saturday, 24 August 2013

NDAMA WA AJABU AZALIWA HUKO NEW ZEALAND, ANA MIGUU 8, MIILI 2, MASIKIO 4 NA KICHWA KIMOJA

planetchoice.blogspot.com
Ndama wa ajabu aliyezaliwa na badae alikufa

planetchoice.blogspot.com
Mmiliki wa ndama huyo 'Neil Davy" akiwa amembeba ndama huyo akiwa tayari ameshakufa...
Neil Davy aliuambia mtandao wa NZ wa nchini humo kuwa kama yeye asingekuepo wakati ndama huyo akizaliwa basi ng"ombe aliyemzaa ndama huyo naye angekufa kwani alihangaika sana wakati akizaa..

Ilikua ni vigumu kumuangalia wakati alipokua anazaa kwani hali yake ilikua mbaya sana, alikua akipiga kelele kutokana na maumivu aliyokua akiyapata kutokana na ndama mwenyewe alivyo nilihangaika naye sana hadi nikalowa jasho jingi(alisema Devy).
Devy aliongeza kua alidhani Ngombe huyo anazaa mapacha lakini kutokana na sababu ambazo hazikufahamika kikazaliwa kiumbe kama hicho.

0 comments :

Post a Comment