Sunday, 28 July 2013

MSHIRIKI WA BIG BROTHER AFRICA KUTOKA TANZANIA "NANDO" AONDOLEWA KATIKA MASHINDANO (DISQUALIFIED)

Mshiriki katika shindano la big brother Africa kutoka Tanzania "Nando" ameondolewa rasmi katika mashindano hayo kwa madai ya kukiuka masharti ya shindano hilo.... Nando ambaye juzi alikorofishana na Elikem na kutupiana maneno makali ambayo yalifanya ahesabiwe kosa la pili baada ya lile la kwanza la kukutwa na kisu katika party ya Channel O na mbaya zaidi alipomtamkia Elikem kwamba "I feel like stabbing him,, these are n*ggas that deserve to die" Nando pia amekutwa na kosa lingine la tatu ambalo inadaiwa alitunza mkasi chini ya godoro anapolala n ambayo ni kinyume na sheria ya mashindano hayo,, ndipo Biggie alipotamka kwamba Nando ameondolewa katika mashindano.. Elikem nae ahesabiwa kosa la kwanza
Nando

KENYA WAYAAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER AFRICA

Mshiriki kutoka kenya aliekua akibeba taji la nchi hiyo katika mashindano ya Big Brother "ANNABEL" ameyaaga mashindano rasmi usiku wa leo baada ya kuchaguliwa na wenzake... ANNABEL ni kati ya washiriki ambao wamekua nominated mara nyingi katika jumba hilo..
ANNABEL ambaye ana degree mbili amedai ya kwamba anafurahi kurudi nyumbani lakini cha muhimu anaenda kujikita na masomo ya ngazi a juu zaidi(master)...

DIAMOND PLATNUM ATOA PICHA MPYA AKIWA NA ROMMY JONES ENZI ZA UTOTO WAO

Rais wa wasafi na kipenzi cha walimbwende "diamond platnumz" kama ilivyo kawaida yake  ametoa picha zingine akiwa na ndugu yake wa karibu romeo jones enzi za utoto wao...



IMG_0042

SINGLE MPYA YA PETER MSECHU KUTOKA WIKI HII

kaa tayari kuusikiliza pini nyingine kutoka kwa peter mssechu na safari hii kamshirikisha Ally Nipishe wa THT.... Ngoma inaitwa Kibudu na hii ndo cover yake..