Monday 21 July 2014

TAARIFA KUHUSU MIILI YA BINADAMU ILIYOKUTWA ENEO LA BUNJU JIJINI DAR ES SALAAM

Taarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni
kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao
wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu

mdogo uliopo eneo la Mpiji,kata ya Mbweni, wilaya
ya Kinondoni,ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yameonekakana kuvuta
mamia ya wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio
hilo,baadhi ya mashuhuda walipoulizwa wamesema
mabaki hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika
mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Wameongeza kwa kusema mabaki hayo ambayo
yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya
ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono,
mbavu na mafuvu ya vichwa hata hivyo Jeshi la
Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia
mabaki hayo katika gari lao lenye namba za
usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili
ya uchunguzi zaidi.
Tunaendelea na juhudi za kusikiliza tamko kutoka
kwa Jeshi la Polisi juu ya undani wa taarifa
hizo,



Credit: millardayo.com

0 comments :

Post a Comment