Nimeambiwa kuwa kwa sasa kuna watu wa nguvu kibao wanaenda
Samunge,Loliondo na kinachowapeleka sio ishu ya Kikombe cha babu tena
sasa hivi ni madini ya dhahabu ambayo inasemekana yamegundulika eneo
hilo.
Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa watu wanaongezeka kijijini
hapo kwa ajili ya kujipatia madini hayo yanayosemekana yapo katika
mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo
kilichopo jirani na kwa Babu.
Diwani wa Samunge Jackson Sandea amesema kwa sasa kuna zaidi ya watu
4,000 na bado wanaongezeka na kusema kuwa idadi hiyo ya watu inaweza
kuwa zaidi ya kikombe cha babu kwa kipindi kile.
Ingawa eneo rasmi zaidi bado halijatjwa ila inasemakana mbali na
kupatikana kwenye mto huo pia dhahabu hiyo ianapatikana hata kwenye
mashamba ya watu,kwa sasa Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini Alex
Magayane amesema wanajiandaa kwenda kijijini hapo baada ya kupokea
taarifa za kugundulika kwa dhahabu kwenye eneo la Samunge.
Imeandikwa na gazeti la Mwananchi.
1 comments :
waooow....
Post a Comment