Leo February 25 Uongozi wa hospitali
ya taifa muhimbili kwa kushirikiana na maafisa wake wa usalama wamemnasa
daktari feki aliyekuwa akiwatapeli fedha wagonjwa na
watu mbalimbali wanaofika
kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
Taarifa kutoka Muhimbili inasema ni
Tukio la tatu kutokea katika hospitali hiyo ingawa matukio ya namna hiyo
yameshawahi kuripotiwa katika baadhi ya hospitali kubwa za serikali kwa baadhi
ya watu wanaotumia mwavuli wa fani ya udaktari kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Msemaji wa Hospital ya taifa
Muhimbili Aminieli Aligaesha amemtaja Daktari huyo feki kwa jina la Kitano
Mustapha na kubainisha kuwa katika upekuzi uliofanywa na maofisa usalama wa
hospitali hiyo wamemkuta mtuhumiwa akiwa na kadi tatu za kliniki,namba za simu
za madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo huku wakitambua kufanya hivyo ni
kosa kwa mujibu wa sheria zilizopo na kanuni za utabibu.
Daktari huyo feki Kitano Mustapha
amekana kutohusika na utaperi huo kwa wagonjwa mbali mbali wanaofika kupata
huduma za kimatibabu na kusema hawezi kuongea lolote mpaka Mwanasheria wake
awepo.
credit: Millardayo.com
0 comments :
Post a Comment