Meli ya Australia imo njiani
kuelekea Mashariki wa Antarctica kwa ajili ya kukwamua meli ya wanasayansi
iliyokwama kwenye theluji tangu siku ya jumanne.
Awali juhudi za uokoaji zilifanywa
na wavuja theluji wa Uchina na Ufaransa lakini walikwama kutokana na unene wa
theluji..Endelea kusoma hapa chini...
Hata hivyo mwandishi wa habari wa
BBC aliyepo kwenye meli ya utafiti ya Urusi anasema tayari theluji imeanza
kupasuka na kuongeza matumaini ya meli hiyo iliyonasa kujikwamua yenyewe na
kuanza kuondoka.
Wanasayansi wapatao sabini na nne,
watalii na wafanyakazi wa meli wapo kwenye meli hiyo iliyokwama inayoitwa .
Meli hiyo imekuwa ikitumiwa na
taasisi ya Australasian Antarctic Expedition kufuatilia njia mtafiti Douglas
Mawson aliyesafiri kwenye njia hiyo karne iliyopita.
Shokalskiy imejaa chakula cha kutosha
na hakuna hatari hii ni kwa mujibu wa timu ya uokoaji.
Pamoja na kunasa, wanasayansi
wanaendelea na majaribio ya kisayansi, kupima nyuzi joto kuzunguka theluji
iliyoanza kupasuka.
Mamlaka ya Usalama wa Majini ya
Australia ambayo ndio inayoratibu uokoaji imesema kikosi cha uokoaji cha Aurora
Australis kilitarajiwa kuwasili katika eneo meli hiyo iliponasa siku ya
jumapili majira ya saa 9 kwa saa za Afrika Mashariki.
Mitambo mikubwa ya kukata theluji
ina uwezo wa kukata theluji yenye unene wa mita 1.6 na uwezo wa kuzoa theluji
ya ukuta wa mita tatu kuzunguka eneo la Shokalskiy.
Kama operesheni hiyo ya uokaji
itashindikana itabidi helkopa zitumike kuwaokoa.
Source:bbcswahili.com
0 comments :
Post a Comment