KIBOWA ni kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu(yatima).. jina KIBOWA ni ufupisho wa maneno “Kituo Bora cha
Watoto”..Kituo hichi kilichopo Lemara jijini Arusha lina Watoto Takribani 49 na
kimekua kikiendeshwa na
WAnamama wawili
ambao hupitia mihangaiko mingi katika kufanikisha mahitaji ya watoto hawa kwani
ukizingatia hawana chanzo chochote cha kuwaingizia mapato(wanaendesha kwa
kutegemea misaada kutoka kwa watu mbali mbali)..
Katika mengi yaliyosemwa na Walezi wa Kituo hicho ni mahihitaji makubwa ya misaada na walijaribu kutuelezea changamoto nyingi
ambazo wanakutana nazo.. Ni dhahiri kua wengi Tunajua Mazingira halisi ya
watoto kama hawa na inahitaji moyo wa kujitolea ili kufanikisha malengo ya
Watoto hawa ambao wana ndoto za kufika mbali kimaisha..
Pamoja na Mengi yaliyofanywa na wanafunzi hao .pia
walijumuika katika Mlo wa Pamoja na watoto hao…
Tafadhali Ndugu ,Jamaa, Marafiki uliyejisikia
Kuguswa na Maisha ya watoto hawa ..Tunaomba kwa Moyo wa Dhati, mchango/msaada
wako wa aina yoyote ile na kwa Kadri utakavyoweza ili tuweze kufanikisha
malengo mazuri waliyonayo watoto hawa…Tunaomba kama Umeguswa na unajisikia
kutoa chochote Tafadhali Wasiliana na kiongozi atakeyekujulisha jinsi ya
Kufikisha Mchango wako Kwa namba ZIfuatazo..(+255659085236
Gama Mwende)..
Kumbuka: Mchango wako ni wa Msaada sana kwa Watoto
hawa na tunakaribisha mawazo/michango mbali mbali katika kutimiza ndoto za
watoto hawa…
Give
a man fish and you feed him for a Day, Teach a Man How to Fish and you feed him
for a Life Time..
0 comments :
Post a Comment