Monday, 11 November 2013

AUNT EZEKIEL: NILIKWENDA KWA DEMONTE KUSAKA MTOTO..




Stori: Hamida Hassan
Sura ya mauzo katika sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amefunguka kuwa alikwenda Dubai kwa mumewe Sunday Demonte kwa ajili ya kusaka mtoto kwani kwa sasa hatumii kinga kwa sababu anahitaji kuitwa mama..endelea kusoma hapa..

 

Akistorisha na Ijumaa Wikienda mara tu baada ya kutia maguu kwenye ardhi ya Jakayaland mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alilazimika kurudi mapema kutokana na msiba wa rafiki yake kipenzi aliyemtaja kwa jina moja la Sofia, Aunt alisema kuwa kwa sasa muda umefika wa kuzaa.

“Hata mume wangu anatamani sana mtoto, tumekaa na kukubaliana juu ya ishu hiyo hivyo muda wowote naweza kuwa mjamzito, japo siwezi kuweka wazi kama ni tayari au bado kuepuka wanga,” alisema Aunt.

0 comments :

Post a Comment