Zambia imetoa vibali vya kukamatwa
kwa wachezaji wake watatu waliokosa mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mjini
Beijing China. Hata hivyo Zambia ilishindwa na Brazil mabao mawili kwa nunge..
Klabu ya DRC TP Mazembe ilisisitiza
kuwa wachezaji hao Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala
walijeruhiwa na kusababisha mgogoro kati ya shirikisho la soka la Zambia na
serikali ya Zambia.
Baada ya wachezaji hao kufanyiwa
ukaguzi mjini Lusaka, shirikisho la soka la Zambia likasisitiza kuwa bado
wanaweza kusafiri kwenda China kwa mchuano huo,lakini klabu ya Mazembe ambako
wachezaji hao hucheza soka ya kulipwa ikawataka kurejea.
Hatua hiyo ilisababisha serikali ya
Zambia kuingilia kati kwa kuwapokonya wachezaji hao pasi zao za usafiri ili
kuwazuia kwenda kuchezea klabu yao mjini Lubumbashi.
Hata hivyo, wachezaji walifanikiwa
kuvuka mpaka na wanaaminika kuwa nchini DR Congo.
Shirikisho la soka la Zambia
limeandikia barua shirikisho la soka duniani Fifa, na kulalamika kuwa klabu ya
Mazembe haikuwaruhusu wachezaji hao kushirki majukumu yao ya kimataifa.
Zambia ilishindwa kwenye mechi hiyo
ya kimataifa mjini Beijing
Zambia ambao ni mabingwa wa kombe la
taifa bingwa Afrika walikuwa wanashirki mechi yao ya kwanza wakiongozwa na
kocha wao mpya Patrice Beaumelle, ambaye alichukua usukani siku nane zilizopita
baada ya Herve Renard kucha kazi.
0 comments :
Post a Comment