Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani, Nelson
Mandela, ametolewa hospitali
ambako amekuwa akitibiwa mapafu tangu mwezi wa
Juni.Taarifa katika tovuti ya rais wa Afrika Kusini imeeleza kuwa Bwana Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwengine inabadilika.
Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.
Nyumba ya Bwana Mandela imebadilishwa ili kumruhusu kupata matibabu ya mgonjwa mahtuti akiwa nyumbani.
Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.
0 comments :
Post a Comment