Mtu mmoja anahofiwa kuuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi kati ya polisi na watu waliobeba silaha hatari ambao wamewateka nyara wateja ndani ya jengo lenya maduka duka la Westgate Shopping Mall katika mtaa wa Westlands, Nairobi.
Hadi sasa hakuna maelezo yoyote kuhusu lengo la washambuliaji hao ingawa taarifa za Polisi zinanazungumzia uwezekano kua ni shambulio la kigadi.
Mkuu wa polisi David Kimaiyo anaongoza juhudi za kuwaokoa mateka wanaozuliwa ndani ya jengo hilo..
Kimaiyo akitumia mtandao wa twitter anasema jengo hilo limezingirwa na polisi . Na polisi wameweza kudhibiti sehemu ya chini ya jengo. Na amewataka watu wsilisogelee eneo hilo.
Source: www.bbcswahili.com
0 comments :
Post a Comment