Mwanamume mmoja nchini Uingereza katika kitongoji cha Middlesbrough,
aliyejidai kuwa
mwanamuziki maarufu duniani , Justin Bieber, ili kuwahadaa
watoto kuweza kumtumia kanda za video wakiwa wanafanya vitendo vya ngono,
amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Robert Hunter, mwenye umri wa miaka 35, na ambaye alijidai kuwa 'Justin
Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana mmoja kutoka Tasmania kufahamisha
polisi kumhusu.
Polisi walimkamata nyumbani kwake akiwa na kanda 800 za video kutoka kote
duniani , baadhi kutoka kwa wasichana na nyengine kutoka kwa wavulana.
Hunter alikubali mashtaka yote 15 yakiwemo kuwachochea watoto kujihusisha
na vitendo vya ngono na kutengeza kanda za video zenye picha chafu.
Mahakama ilifahamishwa kuwa kwa miaka mingi Hunter aliwalenga mamia ya
wasichana kutoka Uingereza, Ufaransa , Spain, Italy, Serbia, Bara Asia na
Canada.
Wasichana walioamini kuwa mwanamume huyo alikuwa kweli Justin Bieber,
walijipiga picha wakiwa uchi baada ya Hunter kuwaahidi kuwa angekuwa na
uhusiano wa kimapenzi nao.
Kwa mujibu wa kiongozi wa mashtaka Richard Bennet, vijana wa shule pia
walinaswa katika mtego wa Hunter aliyejidai kuwa msichana na kuwataka wafanye
vivyo hivyo ambapo alitumia kanda zao kuwatega wasichana wengine.Lakini walipojaribu kujiondoa kwa mtego wake aliwatumia vitisho.
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 12, alijikata mikono yake baada ya Hunter kuchapisha picha zake kwenye mtandao akiwa uchi pamoja na anwani yake na nambari zake za simu.
Jaji alisema hii ni kesi mbaya kuwahi kuisikia kuhusu udhalilishaji wa watoto kwenye Internet.
0 comments :
Post a Comment