Monday, 2 September 2013

ARSENAL YAKUBALI KUMSAJILI MESUT OZIL KWA PAUNDI 42.4..IKIWA NI REKODI MPYA KWA CLUB HIYO



Arsenal wamekubali dili la kumsajili Messut Ozil kwa paundi 42.4 million ambayo itavunja rekodi ya
club hiyo (rekodi iliyopo kwa sasa paundi 27.4m).
Mchezaji huyo (miaka 24) amekubali kujiunga na timu hiyo lakini inabidi apatiwe vipimo kwanza kabla arsenal haijamtangaza rasmi kua ni mchezaji wao..Ozil atafanya vipimo nchini kwao ujerumani.
Arsenal pia wako katika maongezi ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea “Demba BA (28)” kwa mkopo na pia wanamtaka golikipa wa Parlemo “Emiliano Viviano (27)”
Arsenal wameshindwa kwa kiasi kikubwa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool “Luis Suarez” na mchezaji wa zamani wa Real madrid “Gonzalo Higuain”..
Mpaka sasa Arsenal imefanya usajili wa wachezaji wawili, Straika “Yaya Sanogo (20) ” na midfilder “Mathieu Flamini”
Je Arsenal wataweza kumsajili mshambuliaji huyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo(jumatatu sep 2)?
Source:bbcnews.com

0 comments :

Post a Comment