Lile shindano la kumsaka mkali wa bongo "Epiq Bongo Star Search' kwa mwaka huu wa 2013 hautorushwa ITV kama ilivyokua kawaida na badala yake litarushwa katika kituo cha TBC 1.
Madam Rita ambaye ni jaji mkuu na mwanzilishi wa shindano hilo ametoa sababu za kuhamisha mashindano hayo kutoka ITV na kuyapeleka TBC 1
Kupitia account yake ya facebook, Madam Rita ametoa sababu mbili za yeye kuhamishia shindano hilo TBC 1,, kwanza kabisa madam Rita amedai ya kua ameamua hivyo kwa sababu za kibiashara na pili amedai ya kua ni sababu ya mfumo wa digitali unaotumika nchini tofauti na miaka ya nyuma na TBC 1 inapatikana karibia katika kila king"amuzi ikiwa ni pamoja na DSTV
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment