Mchezaji Mrisho Khalfan Ngasa ambaye usajili wake ulikua na utata baada ya kuonekana kusajiliwa na timu mbili zinazoshiriki ligi kuu.. Usajili wa Ngassa ulileta utata baada ya kuonekana kasajiliwa na timu ya Yanga na Simba.. Leo shirikisho la soka Tanzania "TFF" imemtangaza mchezaji huyo kua ni mchezaji halali wa timu ya yanga.
Mbali na hayo pia mchezaji huyo ambae aliichezea simba msimu uliopita ametakiwa kulipa million
30 alizopokea kutoka kwa timu ya simba na shilingi millioni 15 kama faini. Ngassa pia amefungiwa mechi sita za ligi kuu ikiwemo mechi ya ngao ya hisani ambapo yanga itacheza na Azam siku ya kesho. Ngassa ametakiwa kulipa hizo fedha ndani ya miezi sita na tofauti na hapo atafungiwa kucheza ligi kuu
Edinburgh Hogmanay celebrations cancelled
11 minutes ago
0 comments :
Post a Comment