Mzee Ngurumo(katikati)
Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Maalim Gurumo amestaafu
rasmi kazi ya muziki alioifanya kwa muda wa miaka 53.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
“Muziki kwangu umekuwa kama asili
yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki
kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri
wangu,”alisema Mzee Gurumo.
Pamoja na kufanya kazi ya muziki
Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba
anayoishi na familia yake.
“Mimi nimeimba
kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo. Hata hivyo
alisema nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.
Vilevile Mzee nGurumo amewaasa
vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani kwani ndio chimbuko la
bongofleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu
kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.
Mzee NGurumo ambaye
ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki alifanikiwa
kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein Jumbe na Hassani
Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na Nassibu Abdul
’Diamond’.
Mwanamuziki huyo mkongwe alianza
kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960 ambapo mwaka
1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz na Mlimani Park.
Alidumu na Mlimani Park mpaka
mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na
kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa alipoamua kutangaza rasmi kustaafu kazi
hiyo ya Kimuziki.
0 comments :
Post a Comment