Idadi ya collabo za wasanii wa Afrika, hasa Nigeria na
mastaa wakubwa wa Marekani zinazidi kuongezeka.
Baada ya Wizkid kuthibitisha kufanya collabo na Chris
Brown na Rihanna, P-Square na T.I, sasa mshindi wa
tuzo 2 za MTV (MAMA) na BET 2014, Davido nae
amefunguka kuhusu collabo yake inayokuja na marapper
wakubwa wa Marekani.
Davido ameuambia mtandao NEW AGE exclusively kuwa,
anatarajia kufanya collabo na bosi wa MMG, Rick Rozay
pamoja na ‘label mate’ wake Meek Mill ‘soon’.
“For now I cannot reveal much, but I can definitely tell
you that Rick Ross and Meek Mill are on the cards for
collaborations.” Davido aliuambia mtandao huo.
Pia kupitia Facebook Davido ameandika:
“Hot new collaboration coming out.Are you guys ready
to see this? #RickRoss #MeekMill #HKNGang #MMG”
na kushare link ya habari hiyo.
Hivi karibuni Davido alipokuwa Marekani alipost picha
akiwa na Meek Mill, so inaonekana huo ulikuwa ni
mwanzo wa mipango hiyo mikubwa inayokuja.
0 comments :
Post a Comment