Jana (November 21) B’Hitz Music Group iliweka
wazi uamuzi wa kuwaondoa kwenye label hiyo wasanii watatu ambao ni Vanessa
Mdee, Mabeste na Gosby.
Japokuwa Vanessa na Mabeste walitangaza wiki
hii kujitoa kwenye label hiyo, huku Gosby akiwa bado hajasema chochote, timu ya
BHits imesema kuwa wasanii hao waliondolewa kwenye label hiyo miezi miwili
iliyopita japokuwa hawaamua kutangaza.
Mabeste aliiambia Times fm kuwa ameamua
kujiondoa katika label hiyo kwa kuwa muziki wake ulikuwa haumlipi na kwamba
maisha aliyokuwa anaishi ndiyo yaliyopelekea yeye kudhaniwa kuwa anafanya show
za nje, na kwamba amechoka kuwa mzigo kwao.
Tovuti ya Times fm ilimtafuta Amani Joachim
ambaye ni mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits Music Group ili
kufahamu kuhusu sababu alizozitoa Mabeste kwa upande wa B’Hits, na mikataba
ikoje na kama watachukua hatua zozote za kisheria.
“Hiyo statement ambayo Mabeste ameamua
kuisema kwangu mimi naona haiko sawa kabisa. Sisi ni ndugu na tulikuwa tunaishi
hivyo, tatizo la mtu mmoja ni tatizo la mtu mwingine yaani tunakuwa pamoja
kabisa. Na kuna vitu vingi ambavyo Mabeste anajua kwamba tunavifumbia macho.
Hata hiyo mikataba, sisi na Mabeste kuna kipindi tume-deal hata bila mikataba
na mambo yakawa safi tu kwa sababu kuna ile heshima na kuaminiana.” Amesema
Amani.
Ameyaelezea pia madai ya Mabeste kuwa
mabadiliko yake katika maisha ndiyo yaliyosababisha B’Hits kuhisi kwamba
anapiga shows za nje.
“Mabeste inabidi aangalie statements zake, na
muda ambao anaamua kutoa hizo kauli kwa sababu kati yetu sisi tuna siri nyingi
sana (Mabeste na Upande wa B’Hits). Tusifike sehemu kwamba tukaanza kufaidisha
kila mtu, hicho ndicho kitu ambacho ningependa kukiweka sawa. Hizo shows na
vitu vingine ambavyo labda alikuwa anavifanya akiwa nje tunavifahamu vingi tu,
lakini kutokana na ule u-brother na nini tunavichunia tu.” Ameeleza kiongozi
huyo wa B Hits.
Hata hivyo Amani amekubaliana na kuwepo kwa
ubovu wa soko la muziki ambapo amesema hata shows zikiwepo bado malipo yanayotolewa
yako chini kiasi kwamba Kampuni haliwezi kuendeshwa kwa kutegemea kugawana
kipato hicho na msanii.
Aliongelea pia madai ya Mabeste kuwa B’Hits
haikuwa inamfanya atengeneze pesa kupitia muziki wake.
“Well, hopefully kule anakoenda atapata.
Tunaelewa Mabeste ana majukumu, maisha yake tunajua kwamba yamebadilika kwa
namna flani. Personally nafahamu, sijui akina Harmy na Pancho. That’s why I’m
ready to stay quiet kwenye vitu kama hivyo, nilikuwa tayari kukaa kimya…sina
haja ya kufunguka ni vitu vingapi ambavyo Mabeste ameshafanyiwa katika hali ya
u-brother, I will not say them kwa sababu kipindi mimi navifanya nilivifanya
katika good will na nilitaka iishie hivyo, Amani will never say them.”
C.E.O wa B'Hits Hermy B aliuambia mtandao wa
Bongo5 kuwa Vanessa, Gosby na Mabeste hawana shukurani kwa kile ambacho B Hits
imewafanyia na kutoa mfano kuwa alitoa shilingi million nane mfukoni kulipia
video ya Closer ya Vanessa na kiasi kingine kulipia kazi alizofanya nje
ya studio za B Hits, fedha ambazo hazijawahi kurudi.
Nae Amani Joachim alitoa ushauri kwa Vanessa,
Mabeste na Gosby kwa ujumla kuwa wawe na amani na waendelee kufanya mambo yao
na kuacha kutengeneza vita kati yao na B’Hits kupitia media kwa kuwa hata yeye
ameamua kuyafumbia macho mengi.
Lakini vipi kuhusu hasara ambayo B’Hits
itaipata kutokana na kuondoka kwa wasanii hao kwa kuwa walichukuliwa wakiwa
hawana majina na wakati huu wanaondoka wakati wameanza kuwa productive.
Mwana sheria na Chief Operations Officer wa
B’Hits anaeleza.
“They were real productive na naweza
kukwambia kweli hawa watu wako very talented, na B’Hits haijawahi kum-house mtu
ambaye ni mbovu, na ndo maana watu wanashangaa kwa nini mna nyumba kubwa ya
media halafu mna watu watatu tu, sisi kuna kipindi tulikuwa na msanii mmoja tu
Mabeste for like 4 years, ni kwa sababu tunaangalia talent.
“Na kusema kwamba sasa hivi tutakuwa
hatujarudi nyuma utakuwa ni uongo, kuondoka kwao ndio tutarudi nyuma steps
kadhaa, lakini pia kutokana kwamba plans tulizopanga kufanya wakati tukiwa nao
zilikuwa hazijafika kuiva, we are ready to do that with someone else, Mungu
hajagawa kipaji kwa watu wawili au watatu.”
Amesema anaamini baada ya Gosby, Vanessa, na
Mabeste watakuja watu wengine ambao wana vipaji pia.
Kauli ambayo inaungana na ile ya Hermy B kuwa
B’Hits itatangaza wasanii wapya wa label hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu kutoka
kwa mwana sheria huyo kuhusu mkataba kati ya B’Hitz na wasanii hao na
damages/athari za kuvunja mkataba huo zikoje na iwapo watawadai wasanii hao.
Amesema mikataba ilikuwa tight lakini kwa
mazingira ya Tanzania na hali halisi ya kipato cha wasanii wa Tanzania hiyo
mikataba inakuwa kama useless kwa kuwa kiasi kinachotakiwa kulipwa na msanii
huyo ni kikubwa kuliko hali halisi ya maisha ya msanii husika.
“Ukimchukua bwana mti ukampeleka mahakamani,
mahakama inaangalia damage ambayo imeingia katika kampuni, na mwisho wa siku
inachukua maamuzi ambapo itakwambia bwana mti kama amepatikana na kosa amlipe
bwana jose million 150 Kwa mfano, haimfungi. Problem ni kwamba bwana mti hana
hata shilling 200 mfukoni mwake, we unadhani utamfanyaje bwana mti?” Alieleza
kwa mfano.
“Kwa sababu mahakama ikishakupa judgement
inakuacha ukatafute hiyo hela, haimfungi mtu. Kesi za madai sio kesi za
jinai..sasa hapo imagine hapo ni wasanii wangapi leo unawafanyia kazi ya
million 40 Million 50, ambayo ukiingia katika intellectual property court
(mahakama ya maswala ya copy right), na copy right ni very expensive,
tunaongelea six figures, eight figures. Sasa angalia ni wasanii wangapi hapa
Tanzania wanaweza kukulipa eight figures.?” Amesema.
Kutokana na hali hiyo amesisitiza kuwa kuna
haja ya kuwalipa wasanii pesa nyingi katika kazi zao huko wanakoenda kufanya
ili wanapopata matatizo waweze kulipa, na kwamba bila hivyo mikataba ya label
na wasanii Tanzania itakuwa useless.
Hii inamaanisha kuwa hakuna hatua zozote za
kisheria ambazo B’hits itachukua kudai fidia kutoka kwa wasanii hao.
Hata hivyo uongozi wa B’Hits umesema utaachia
nyimbo nyingine za wasanii hao zilizoko studio na kwamba zitachezwa redioni,
lakini wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia kwa kuwa ni mali halali ya
kampuni hiyo.
0 comments :
Post a Comment