Serikali ya Tanzania imekosoa
Muungano mpya wa hiari wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda ulioundwa hivi
karibuni.
Serikali ya Tanzania imeuelezea kuwa
unaenda kinyume na makubaliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na
Rwanda walikutana hivi Karibuni nchini Uganda ambapo walikubaliana kuanzisha
miradi ya pamoja ya kimaendeleo katika nchi zao hatua ambayo haijapokelewa vema
na Serikali ya Tanzania
Hii ni ishara ya hivi karibuni
kuwepo kwa mgawanyiko katika nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hii si mara ya kwanza kuzuka tofauti
katika Jumuiya hii ambayo imeundwa ikiwa ni mara ya pili baada ya ile ya awali
kuvunjika mwaka 1977 ,wakati huo ikiwa na wanachama watatu tu yaani
Tanzania,Kenya na Uganda.
Mgogoro huu wa sasa inaelezwa kuwa
chanzo chake ni mkutano wa pande tatu uliofanyika mapema mwezi July mwaka huu
nchini Uganda ambapo nchi za Kenya,Uganda na Rwanda zilikubaliana kuungana
katika kufanya miradi ya kimaendeleo ya pamoja ndani ya nchi zao,muungano ambao
unaonekana kuitenga Tanzania,huku Burundi hivi karibuni nayo ikijiunga na
Muuungano huo na kuufanya kuwa wa nchi nne.
Tanzania inasisitiza kuwa kulipaswa
kuwepo na mazungumzo na maafikiano miongoni mwa nchi wanachama kabla ya kuanza
utekelezaji wake.
Katika taarifa iliyotolewa na Wizara
ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imetaja kuwa nchi hizo zimekiuka makubaliano
yaliyoko kwenye mkataba wa jumuiya hiyo.
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki yenye makao yake Makuu mjini Arusha haijasema lolote tangu kuanza
Muungano huo wa nchi tatu na wala haijajibu malalamiko hayo ya Serikali ya
Tanzania.
bbcswahili.com
bbcswahili.com
0 comments :
Post a Comment